Monday 21 August 2017

Yanga yawaweka adharani wachezaji watakao ukosa mchezo wao na Simba.

Image result for dismas ten
Dismas Ten afisa Habari wa klabu ya Yanga.
Klabu ya Yanga ambayo inatarajiwa kuingia nchini siku ya Jumanne ya tarehe 22 Agosti mwaka huu ikitokea visiwani Pemba Zanzibar ilipoweka kambi ya wiki nzima kujiandaa dhidi ya Simba imesema wachezaji wake watatu akiwepo Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa , Benno Kakolanya na Mwasiuya kutokana na kuwa majeruhi.

Aidha klabu hiyo imesema kuwa imejipanga tayari kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya wapinzani wake wa jadi na kusema hali kikosini iko salama wanasubiri mchezo husika ambao utapigwa siku ya Jumatano tarehe 23 Agosti uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. 

Katika mitandao ya jamii bado tambo mbalimbali zimekuwa zikiendelea dhidi ya watani hao wajadi huku kila upande ukijigamba kuwa katika mchezo huo wao wataibuka na ushindi wa hali ya juu, huku wengine wakidai kuwa huenda Simba inaweza kurudi historia yake ya kuifunga Yanga kwa goli nyingi, wakati washabiki wa Yanga wao wanajigamba kuwa mwaka huu tena ubingwa unarudi Jangwani.

No comments:

Post a Comment