Shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza kikosi bora cha soka ya wanaume duniani mwaka 2017 ambapo kuna mabadiliko matatu kutoka kwa kikosi kilichotangazwa mwaka 2016.
Kwenye kikosi hicho, maarufu kama Fifpro World XI, mlindalango Gianluigi Buffon amechukua nafasi ya Manuel Neuer, naye beki wa AC Milan Leonardo Bonucci akachukua nafasi ya kigogo wa Barcelona Gerard Pique kwenye safu ya ulinzi.
Mshambuliaji wa PSG Neymar, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi duniani naye ameingia nafasi ya Luis Suarez katika safu ya mashambulizi.
Kikosi hicho kina wachezaji watano kutoka Real Madrid, wawili wa Barcelona, wawili wa PSG, mmoja wa Juventus na mmoja kutoka AC Milan.
Hakuna mchezaji hata mmoja wa Ligi ya Premia aliyefanikiwa kujumuishwa katika kikosi hicho.
(Formation 4-3-3)
Gianluigi Buffon
Dani Alves, Marcelo, Sergio Ramos, Leonardo Bonucci
Luka Modric, Toni Kroos, Andres Iniesta
Lionel Messi, Neymar, Cristiano Ronaldo
Mkufunzi bora duniani soka ya wanaume
Zinedine Zidane amemshinda meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya kuongoza Real Madrid kushinda La Liga msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu 2012 na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mtawalia msimu uliopita.
Conte alishinda Ligi ya Premia msimu uliopita.
Massimiliano Allegri wa Juventus, ambaye aliongoza klabu yake kushinda Serie A na Coppa Italia msimu uliopita alikuwa wa tatu.
Mkufunzi bora soka ya wanaume | ||
---|---|---|
Zinedine Zidane - 46.22% | Antonio Conte - 11.62% | Massimiliano Allegri - 8.78% |
Mkufunzi bora duniani soka ya wanawake
Kocha wa Uholanzi Wiegman aliyeongoza Uholanzi kushinda Euro 2017 nyumbani kwao amechukua taji hilo.
Waliwalaza Denmark kwenye fainali
Mkufunzi bora wa soka ya wanawake | ||
---|---|---|
Sarina Wiegman - 36.24% | Nils Nielsen - 12.64% | Gerard Precheur - 9.37% |
No comments:
Post a Comment