Kiungo wa Simba Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amesema kwamba baada ya mchezo wao dhidi ya Lipuli anatarajia kwenda nyumbani kwa kwa ajili ya kuhani misiba ya ndugu zake ikiwemo aliyekuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, Hamad Ndikumana.
Ndikumana amefariki dunia hivi karibuni wakati kiungo huyo akiwa kwenye majukumu ya klabu yake katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara waliocheza mkoani Mbeya.
Niyonzima amesema kwamba, alitakiwa kuondoka jana Jumanne lakini hakuweza hivyo hadi ahakikishe anamaliza mchezo wao dhidi ya Lipuli FC, utakaochezwa Jumapili hii katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
“Nilitakiwa leo Jumanne (jana), niende Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria kwenye misiba kama mitatu hivi iliyotokea nikiwa Mbeya kwenye majukumu ya klabu yetu, maana kama unakumbuka kwenye mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Mbeya City nilifiwa na mama yangu mlezi.
“Lakini pia siku chache kabla ya kukutana na Prisons katika mchezo wetu wa Jumamosi iliyopita nilipata misiba miwili tena kwa mkupuo, ambapo ndugu yangu kabisa Hamad Ndikumana alifariki dunia pamoja na mchezji mwezangu wa timu ya taifa naye alifariki ghafla jambo ambalo kwa namna moja au nyingine limeniuma hivyo lazima niende,”alisema Niyonzima.
No comments:
Post a Comment