Wednesday, 22 November 2017

Nyota wa Yanga wa Amissi Tambwe aanza rasmi Mazoezi.

Image result for Amissi Tambwe mazoezini
Hatimaye mshambuliaji nyota wa Yanga, Amissi Tambwe ameanza mazoezi na wenzake.

Tambwe ambaye hajacheza hata mechi moja ya Ligi Kuu Bara msimu huu, leo ameanza mazoezi na wenzake wakati Yanga ikijifua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Awali, kwa takribani siku nne, Tambwe amekuwa akizunguka uwanja peke yake wakati wenzake wakiendelea na mazoezi.

Lakini leo amejumuika na wenzake katika mazoezi na ameonyesha kuwa yuko vizuri kutokana na kushiriki katika zoezi la upigaji mashuti.

Tambwe amekuwa kati ya wachezaji waliopiga mashuti makali katika mazoezi ya leo.

No comments:

Post a Comment