Friday 24 November 2017

HIVI PUNDE:Mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama afariki Dunia.

Related image
Taarifa za  uthibitisho wa  kifo cha mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama  ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.


Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment