Friday 24 November 2017

Mchezaji Mbrazil Robinho kwenda jela kwa kosa la Ubakaji

Related image
Mahakama ya Italia, imemhukumu Kiungo mshambuliaji wa zamani wa AC Milan, Robinho de Souza kwenda jela miaka tisa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ubakaji.

Robinho amepatikana na hatia ya ubakaji ya dada wa miaka 22, wakati huo akiwa anaitumikia AC Milan.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya wanasheria wake pamoja na watuhumiwa wengine walioshitakiwa na Robinho ambao walielezwa kushirikiana kumbaka dada huyo raia wa Albania wakati huo akiwa na miaka 22.
Robinho is a Brazil international - and has won 100 caps after making his debut in 2003
Robinho aliyewahi kuichezea Real Madrid na Manchester City hatarudishwa Italia kwa kifungo hadi hapo atakapokata rufaa au la.

No comments:

Post a Comment