Tuesday, 5 December 2017

Jeshi la Polisi lamshikilia Mwanafunzi aliyesambaza Picha za Nyufa Hosteli za UDSM.

Image result for lazaro mambosasa
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson anashikiliwa na polisi akituhumiwa kusambaza picha kuonyesha nyufa kwenye majengo ya hosteli.


Dawson ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) alikamatwa jana Jumatatu Desemba 4,2017 mchana.

Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo jana saa saba mchana.
Kumbusho Dawson.

"Ni kweli Kumbusho alikamatwa jana mchana  na kupelekwa kituo cha polisi cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri polisi walisema hawana uwezo wa kumuhoji hapa hivyo wakampeleka Oysterbay," amesema Anastazia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipotafutwa amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo. Alisema anasubiri atakapofikishiwa taarifa atazitoa kwa umma.

No comments:

Post a Comment