Kwa mara ya pili mashabiki wamelishambulia sanamu la mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi.
Messi ambaye sasa ni nahodha wa Argentina inayojulikana kama Albiceleste, sanamu lake limeshambuliajiwa na kuvunjwa kwa mara ya pili jijini Buones Aires huko Argentina.
Haijajulikana sanamu hilo limefanyiwa hivyo na watu gani lakini hii ni mara ya pili tokea mwaka 2016 lilipozinduliwa.
Pamoja na Messi kuwa tegemeo la Argentina na pia anaitangaza nchi hiyo, mashabiki wengi wamekuwa hawana furaha kutokana na kitendo chake cha kushindwa kuipa timu hiyo Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment