Tuesday 5 December 2017

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ampa onyo Donald Trump.

Image result for emmanuel macron and donald trump
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemuambia Donald Trump kuwa ana wasiwasi kuwa rais huyo wa Marekani anaweza kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Uamuzi wowote kuwa mji huo unastahili kuwa katika viwango vya mazungumzo kati ya Israel na Palestina, Bw Macron alisema.
Mapema onyo kama hilo lilitolewa na nchi za kiarabu na mataifa ya kiislamu.
Ripoti zinasema kuwa rais wa Mareknia atautambua mji wa Jerusalem kuwa mji wa mkuu wa Israel.
Israel na Palestina wote wanadai kuwa mji huo ni mji wao mkuu.
Ikulu ya White House ilisema kuwa anaweza kukosa siku ya mwisho ya Jumamosi kuweka sahhihi agizo la kuzuia kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Avivi kwenda Jerusalem.
Kila rais akiwemo Trump ametia sahihi agizo kila baada ya miezi sita tangu bunge le Congress lipitishe mswada mwaka 1995 wa kutaka ubalozi huo kumamsihwa,
Hali ya mji wa Jerusalem ndio channzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina wanaoungwa mkono na nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiislamu.

No comments:

Post a Comment