Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa na kuachiliwa kwa dhamana, denti Dawson Kumbusho, ambaye ni mbunge wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa kosa la uzushiwa kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii na kusambaza picha za jengo la bweni la chuo hicho lenye nyufa.
Akizungumza na wanahabari leo, ofisini kwake. Kamanda Mambosasa amesema kuwa waliamua kumkamata denti huyo kwa kosa la kusambaza picha zile kinyume na sheria.
Kama angekuwa muungwana alipaswa kuwasiliana na wamiliki wa jengo lile. Hata hivyo, kwa sasa ameaachiwa kwa dhamana.
“Sisi kama jeshi la polisi baada ya kusambaa kwa picha zile tulimshikilia mwanafunzi huyo kwa ajili ya kumuhoji baada ya kupata kile tulichokuwa tunakihitaji, ameruhusiwa kupewa dhamana na sasa yuko nje,” alisema Kamanda Mambosasa.
No comments:
Post a Comment