MAHAKAMA Kuu imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyokuwa imemuachia huru katika kesi ya kutoa maneno ya uchochezi.
“Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na mimi nakubaliana na uamuzi huo, hivyo namuachia huru,” amesema Jaji Mkasimongwa.
Aidha Jaji Mkasimongwa amefafanua kwamba upande Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.
Mnamo Agosti 10, 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, inadaiwa kwamba Ponda alitoa kauli za kichochezi kwa waumini wa Kiislam ambapo mojawapo ya kauli ni ile aliyosema kwamba (Waislam) wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
No comments:
Post a Comment