FC Barcelona wameweka msisitizo kwamba hawatawapigia makofi ya heshima ya ubingwa wa Kombe la Dunia wapinzani wao Real Madrid timu hizo zitakapokutana katika El Clasico Jumamosi hii.
Barcelona imesema haiwezi kufanya hivyo kwa Madrid kubeba ubingwa wa dunia.
Wameeleza, wanatambua kama ingekuwa wamebeba ubingwa wa La Liga au Ligi ya Mabingwa na mechi inayofuatia wakawa wanakutana, wangeweza kufanya hivyo.
Kwa kuwa wamechukua ubingwa wa dunia, huo hauko katika utararibu wa kufanya hivyo na wao watashikilia hilo.
No comments:
Post a Comment