Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umeanza Mjini Dodoma ambapo utafanyika kwa siku mbili, Desemba 18-19, 2017 ambapo Mkutano huo umebeba ajenda kuu ya kukamilisha uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaanza leo bila kuwa na shamrashamra zilizozoeleka katika mikutano iliyopita.
Wakati idadi ya wapambe ikiwa ndogo tofauti na miaka iliyopita, hata wajumbe wanaowania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) nao walionekana wachache, huku wakitumia zaidi mitandao ya kijamii kujinadi.
Akizungumza wakati wa akifungua Rasmi Mkutano huo, Rais Magufuli amekisifu chama chake kwa (CCM) kwa ushindi mnono walioupata kwenye uchaguzi mdogo wa kata 43 uliofanyika hivi karibuni ambapo CCM waliibuka washindi kwa kata 42.
“Chama chetu kimeshinda kata 42 na kiti kimoja kikatuponyoka kwa mbali, nawapongeza kwa ushindi tulioupata. Ushindi huo umetopkana na mambo haya.
“Uungwaji mkono wa chama chetu na kukubarika katika jamii, uimara na ukomavu wa chama hiki ambapo tangu kiundwe kimeongoza dola miaka yote tangu kilipoanzishwa mwaka 1977, tunatekeleza kwa vitendo mambo tunayoyaahidi kwa vitendo wakati wa kampeni na mwisho tumeshinda kwa vile CCM tuna umoja na mshikamano,” alisema Magufuli.
“Sina uhakika kama kuna chama kingine ambacho waanzilishi wake wote wapo, hapa yupo Mzee Mwinyi (Rais Mstaafu, Mzee Kikwete, Mzee Mkapa, Mzee Makamba, Mama Kikwete, Mama Mwinyi,” aliongeza Magufuli.
No comments:
Post a Comment