Thursday 21 December 2017

Man United yatupwa nje ya michuano Chelsea yatinga nusu Fainali.

Bristol City 2-1 Man United: Pogba and Ibrahimovic humbled
Klabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao kwa kuwaondosha mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Manchester United.

Bristol walianza kuzifumania nyavu za United kwa goli la Joe Bryan, katika dakika ya 51 ya mchezo iliwchukua dakika saba tu kwa Manchester United, kusawazisha goli hilo kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic.
Shujaa wa Bristol City alikuwa ni kiungo Korey Smith aliyefunga goli la ushindi katika dakika za lala salama.
Nayo Chelsea wakatinga katika hatua ya nusu fainali kwa kuwatungua AFC Bournemouth kwa magoli 2-1 .

chelseaHaki miliki ya picha
Image captionMfungaji wa bao la Chelsea

Kiungo Willian Borges da Silva, ndie aliyeanza kupatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 13 ya mchezo
Bournemouth wakasawazisha goli hilo katika dakika ya tisini kupitia kwa kiungo Daniel Gosling, Mshambuliaji hatari wa Chelsea Alvaro Morata akawapeleka Chelsea nusu fainali kwa goli la dakika ya 91.
Michezo ya nusu fainali itapigwa januari 9, mwakani kwa Chelsea kucheza na Arsenal na Bristol City kucheza na Manchester City.

No comments:

Post a Comment