Naibu wa waziri mkuu wa Uingereza, Damian Green, ameachishwa kazi baada ya kubainika kuwa alikiuka kanuni za uwaziri.
Bwana Green ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Waziri mkuu Theresa May alibainika kuwa alitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu picha za ngono zilizokutwa kwenye komputa yake ya ofisini.
Damian Green alikuwa anachunguzwa pia juu ya madai ya kutowaheshimu wanawake wanaharakati katika chama chake cha Conservative.
Hata hivyo kiongozi huyo amekanusha kuhusika na mashitaka yote yanaomkabili.
Mhariri wa masuala ya kisiasa wa BBC, amesema kuondoka kwa kiongozi huyo ni pigo kuwa kwa waziri mkuu
No comments:
Post a Comment