Tuesday, 19 December 2017

Yanga warudi tena kivingine.

Image result for yanga warudi mazoezini
Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini tena, safari hii kikianzia gym.

Yanga wameanza mazoezi leo wakijifua kupitia gym na kesho wanatarajia kurejea uwanjani.

Wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja baada ya sare ya bila kufungana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania.

Pamoja na sare, Yanga walionekana kufarijika baada ya wachezaji wake wawili, kiungo Papy Tshishimbi na Mrundi, Amissi Tambwe kurejea uwanjani na kucheza mechi tena.

Yanga imekuwa ikisumbuliwa na majeruhi mfululizo lakini kocha George Lwandamina amekuwa akipambana kuhakikisha wanakuwa katika mwendo mzuri.

No comments:

Post a Comment