Wakati Simba ikitarajia kucheza michuano ya kimataifa mapema mwezi ujao dhidi Gendarmerie Tnale ya Djibouti, beki wa timu hiyo, Asante Kwasi amefunguka kuwa wapo fiti na watapambana ingawa kwa sasa hakuna timu ya kudharau.
Simba inatarajiwa kushiriki michuano hiyo baada ya miaka kadhaa kupita huku mara ya mwisho ikiwa ni msimu wa 2012/13 baada ya msimu wa nyuma yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Beki huyo kwa sasa amekuwa chachu ya mafanikio licha ya kutua hivi karibuni ndani ya kikosi hicho ambacho amekitumikia katika mechi mbili za ligi dhidi ya Singida na Kagera Sugar.
Kwasi alisema kuwa wanajipanga kupambana na upande wa kimataifa ni lazima wajitume kwa bidii hasa katika hatua ya awali ili kuweza kusonga mbele na kufanya vyema.
“Najua ni kazi ngumu lakini mechi hizi za kimataifa hakuna timu ya kudharau hata kidogo, sababu siku hizi kila timu inapigana kuhakikisha inapata matokeo mazuri na michuano ile ni lazima kufanya vizuri hasa sisi wachezaji kupata nafasi ya kujitangaza zaidi.
“Kwa upande wangu napambana kuhakikisha nashirikiana na wenzangu vyema ili kuweza kupata matokeo kwa mechi zote ambazo tunaendelea kucheza ili kuwa vizuri,” alisema Kwasi.
No comments:
Post a Comment