Pacha ya ulinzi wa kati inayowahusisha Juuko Murshid na Asante Kwasi imeonekana kumvutia Kocha Pierre Lechantre.
Pacha hiyo hiyo aliiona katika mechi mbili dhidi ya Singida United na Kagera Sugar naye amekuwa akiitumia muda mwingi mazoezini.
Kutokana na hali hiyo, inaonekana wazi Lechantre raia wa Ufaransa ataitumia pacha hiyo katika mechi dhidi ya Majimaji ya Songea.
Mechi hiyo inayochezwa Dar es Salaam inaonekana itakuwa ngumu lakini Lechantre amewaandaa vijana wake kwa ajili ya ushindi.
Kocha huyo Mfaransa anaonekana kuvutiwa na walinzi walio na uwezo wa kupiga vichwa, wepesi wa kuondosha mpira na wanapiga pasi sahihi jambo ambalo Juuko raia wa Uganda na Kwasi kutoka Ghana wako vizuri.
No comments:
Post a Comment