Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia aliahidi hata kabla ya mechi dhidi ya Azam FC kwamba lazima ana bao lake moja.
Chirwa aliwaahidi wachezaji wenzake kwamba lazima angefunga bao moja au mawili dhidi ya Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, jana.
Kweli katika mechi hiyo, Chirwa alifunga bao la kusawazisha lililosaidia Yanga kuituliza Azam FC kwa mabao 2-1.
“Chirwa aliwaambia wachezaji kuwa atafanya kila analoweza ili afunge. Alisisitiza na anaonekana alipania.
“Unajua mara ya mwisho Yanga na Azam yeye ndiye alikuwa amefunga bao,” kilieleza chanzo.
Chirwa ndiyo alikuwa anarejea kutoka katika adhabu ya kusimamishwa na Bodi ya Ligi na akaonyesha uwezo mkubwa.
No comments:
Post a Comment