Thursday 25 January 2018

Majibu ya Takukuru kwa Mahakama kuhusu Upelelezi kesi ya Jamal Mlinzi.

Related image
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema upelelezi dhidi ya aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake umekamilika.

Awali Mahakama ya Kisutu ilitaka Malinzi, katibu mkuu wa zamani wa TFF, Mwesigwa Celestine na aliyekuwa mhasibu wa shirikisho hilo kuhojiwa tena na Takukuru.

Hivyo Takukuru imeiambia mahakama hiyo kwamba tayari upelelezi huo katika kesi inayowakabiri Malinzi na wenzake kwa tuhuma za utakatishaji fedha imekamilika.


Malinzi na wenzake wako mahabusu tokea mwaka jana huku kesi hiyo ikiendelea kuunguruma katika mahakama ya Kisutu.


No comments:

Post a Comment