Thursday 25 January 2018

Kocha Mkuu wa Azam FC Aristica Cioba asema anachotaka kuifanya Yanga.

Image result for Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioba amesema angependa kuzungumza kwa vitendo zaidi kuliko maneno mengi wakati  wakiivaa Yanga Jumamosi.

Yanga itakuwa mgeni wa Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini DAr es Salaam.

Mechi hiyo sasa itapigwa saa 10 jioni na Cioba amesema wamewekeza nguvu zao kwa vitendo wakianza na mazoezi.

“Tunaendelea na mazoezi na tunaangalia wapi tulikosea katika mechi zilizopita na baada ya hapo ni kazi.

“Nafikiri mambo yaelekezwe katika vitendo zaidi na si maneno lakini kikubwa tunataka kushinda siku hiyo,” alisema.

No comments:

Post a Comment