Monday, 29 January 2018

Rais Magufuli atoa heshima za mwisho kwa Jaji Mstaafu Robert Kisanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 28 Januari, 2018 ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga (pichani) nyumbani kwa marehemu Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 

Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa pole kwa mke wa Marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja na familia ya marehemu. 
 
Jaji Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam jana Jumapili Januari 28, 208.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam jana Jumapili Januari 28, 2018.


No comments:

Post a Comment