Monday, 29 January 2018

Sure Boy aweka sawa kuhusu kuipenda Yanga.

Related image
Kiungo mshambuliaji wa Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amesema anawashangaa mashabiki wa timu hiyo wanaodai kuwa yeye ndiyo chanzo cha kufungwa katika mchezo dhidi ya Yanga kwa kuwa ana mpenzi na Yanga, kitu ambacho hakina ukweli wowote zaidi ya kuwa ni uzushi uliokosa tija.
  
Sure Boy kwa sasa ndiyo mchezaji pekee  ambaye amesalia katika timu hiyo tangu ipande Ligi Kuu Bara mwaka 2008 ambapo katika mchezo wa juzi Jumamosi alipata kadi nyekundu dakika ya 81 wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 1-2 dhidi ya Yanga katika  mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Sure Boy amesema kuwa hashangazwi na maneno ya mashabiki hao, kwa kuwa ana miaka kumi mpaka sasa akiitumia timu hiyo na amekuwa akiambiwa siku zote lakini walipaswa kuangalia mwamuzi alivyoweza kuwamaliza mapema katika mchezo huo.

“Unajua kadi imetokea kwa sababu ni sehemu ya mchezo na Hassan Kessy alitumia udhaifu wa mwamuzi kuweza kunitoa kwa kadi nyekundu, lakini sijui kwa nini watu wote hawakuona kitendo cha kijinga alichokifanya Kessy kwa Joseph Mahundi wakati yupo pale chini, matokeo yake wananiangushia lawama mimi.


“Angalia tangu mpira unaanza, tayari mwamuzi alishaonekana hakuwa na usawa kwa timu zote, ametoa zaidi ya kadi tano kwetu halafu Yanga yule Papy Tshishimbi amecheza rafu muda wote na ngumi akarusha mbele yake halafu wanasema mimi nimewasaidia Yanga, kwani bao la pili limefungwa nikiwa wapi, nina miaka kumi nacheza Azam hivyo siwezi kuwashangaa, zaidi naangalia nitaisaidiaje timu huko mbele,” alisema Sure Boy.

No comments:

Post a Comment