Monday, 8 January 2018

Sababu ya Amissi Tambwe kuondolewa Zanzibar na kurudishwa Dar es Salaam.

Image result for Amissi Tambwe
Mshambuliaji Amissi Tambwe mchana wa leo amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi kufuatia kuugua malaria.

Taarifa zinaeleza Tambwe ameondolewa katika kambi ya Yanga mjini  Zanzibar ili kwenda kupatiwa matibabu.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu amethibitisha Tambwe kuondolewa Zanzibar na kurudishwa jijini Dar es Salaam.

"Ana malaria,kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar ili apate matibabu zaidi,” Dr Bavu.

Pamoja na mjadala kwamba kama ni malaria angeweza kutibiwa Zanzibar, Tambwe atapata matibabu jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji huyo amerejea kikosini Yanga hivi karibuni baada ya kukaa nje akiwa majeruhi.

No comments:

Post a Comment