Saturday 27 January 2018

Tetesi zote kubwa kutoka barani Ulaya hii leo Januari 27.

Image result for Eden Hazard, Harry Kane,David de Gea
Real Madrid inamtaka Mauricio Pochettino kuwa mkufunzi wake mpya na tayari imewasiliana na mkufunzi huyo wa Tottenham. (Mail)

Spurs pia inakaribia kukamilisha uhamisho wa dau la £21.9m kusajili winga wa Paris St-Germain na Brazil 25, Lucas Moura. (RMC Sport - in French)
Manchester City imekubali dau la rekodi ya £57m kumsajili beki wa kati wa Athletic Bilbao's ,23, Aymeric Laporte. (Guardian)
Real Madrid inapanga kumnunua mshambuliaji wa Cheslea na Ubelgiji Eden Hazard,27, mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane na kipa wa Manchester United na Uhispania , 27, David de Gea this summer. (Mail)
Arsenal imebadilishana kwa dau la £10m pamoja na beki wake wa kulia mwenye umri wa miaka 32 Mathieu Debuchy kwa beki wa kati wa West Brom na Northern Ireland Jonny Evans. (Star)
The Gunners italazimika kutoa dau la £25m iwapo inataka kumnunua Evans kutoka West Brom(Sun)
Mkufunzi wa West Brom Alan Pardew anasema kuwa klabu inayomtaka Evans itapata majibu mazuri iwapo itawasiliana na timu hiyo wikendi badala ya kuanzisha mazungumzo mwisho wa dirisha la uhamisho siku ya Jumatano.. (Telegraph)
Ombi la Newcastle la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Feynoord na Denmark Nicolai Jorgensen kwa dau la £15m limekataliwa (Sky Sports)
Klabu hiyo ya uholanzi imeambia Newcastle kwamba watalazimika kulipa dau la 25m euros (£21.9m) kumsajili raia huyo wa Dane. (Northern Echo)
Mkufunzi wa Newcastle Rafa Benitez anasema kuwa Aleksandar Mitrovic hatauzwa kwa ligi ya Uingereza. Brighton inadaiwa ilikuwa tayari imewasilisha ombi lake kumnunua mchezaji huyo wa Serbia. (Telegraph)
Mkufunzi wa West Ham David Moyes atajaribu kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 29, iwapo atashindwa kumtia mkobani mahsmabuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 28. (Sun)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa hawezi kumuhakikishia Sturridge kushiriki katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo iwapo atasalia katika klabu hiyo.. (Guardian)
Mkufunzi wa zamani wa Everton na Southampton Ronald Koeman yuko katika mazungumzo na shirikisho la soka la Uholanzi kuhusu kuwa mkufunzi wa timu ya taifa. (VI - in Dutch)
Juventus inamnyatia beki wa Manchester United mwenye umri wa miaka ,28, Matteo Darmian. (Sun)
Chelsea itatafuta mchezaji mwengine iwapo mktaba wa kumsajili mshambulia wa Roma na Bosnia Edin Dzeko hautaafikiwa mwishoni mwa wikendi hii.. (Telegraph)
Ombi la Brighton la kutaka kumsajili beki wa kulia wa klabu ya Luton kwa dau £1.5m James Justin, 19, limekubaliwa na klabu hiyo ya daraja la pili Uingereza.. (Sun)
Nahodha wa klabu ya Fulham ,27, Tom Cairney anataka kuelekea West Ham lakini klabu yake imekataa kumuuza . The Hammers wameripotiwa kwamba wako tayari kulipa dau la £15m kwa kiungo huyo wa kati wa Uskochi. (Sky Sports)
Aston Villa imejiunga na Hull City katika kutafuta saini ya beki wa Aberdeen Scott McKenna. Tayari maombi matatu ya The Tigers kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 yamekataliwa. (Scottish Sun)
Uhusiano kati ya mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte na mzungumzaji wachezaji wanaotaka kujiunga na klabu hiyo ama wanaoondoka Marina Granovskaia wamekuwa katika mgogoro hadi sasa wanamtumia kipa wa zamani wa klabu hiyo Carlo Cudicini kuwasiliana.(Times - subscription required)
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amesema kuwa hawezi kuwa mkufunzi wa kudumu wa klabu hiyo . (Guardian)

No comments:

Post a Comment