Monday 15 January 2018

Tetesi zote za Soka kutoka barani Ulaya Jumatatu ya leo januari 15.

Image result for Jose Mourinho and Antoine Griezmann
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kuacha kumsajili Antoine Griezmann, 26, kutoka Atletico Madrid mwisho wa msimu na hata Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid, ili amsajili Sanchez na kumpa mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki. (Mail on Sunday)

Arsenal wako makini kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan 28, kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamleta mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29, huko Old Trafford. (Guardian)
Manchester City wamejitoa katika makubaliano ya kumsaini Sanchez na pesa zilizoitishwa na ajenti wake. (Goal)
Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux Malcom siku ya Jumapili na wanatarajia kulipa pauni milioni 40 kwa mBrazil huyo wa miaka 20. (Guardian)
Arsenal na Chelsea wanammezea mate mshambuliaji wa Watford raia wa Brazil Richarlison 20. (Sun)
Andy CarrollHaki miliki ya picha
Image captionAndy Carroll
Chelsea bado wako makini kumsaini mshambuliaji wa mwezi Januari kwa mkopo huku Andy Carroll wa West Ham akiwa katika nafasi nzuri wa kusainiwa. (Telegraph)
Manchester United wako tayari kumpa kipa wa miaka 27 David de Gea mkataba mpya amboa utamweka katika klabu hiyo katika taaluma yake yote.(Mirror)
Crystal Palace wana matumaini ya kumaliza kumsaini mshambuliaji wa Fiorentina raia wa Senegal Khouma Babacar 24 kwa pauni milioni 15. (Guardian)
Crystal Palace pia wako kwenye mazungumzo ya kumsaini kipa wa Ipswich Bartosz Bialkowski. Klabu hiyo inataka zaidi ya pauni milioni 4 kwa mchezaji huyo wa miaka 30. (Sun)
David de GeaHaki miliki ya picha
Image captionDavid de Gea
Liverpool wametupilia mbali mpango wa kumsaini wing'a wa Monaco Thomas Lemarbada baada klabu hiyo kuomba pauni milioni 90 kwa mchezaji huyo wa miaka 22. (Times
Borussia Dortmund wanakaribia kutangaza kumsaini beki la Basel mswisi Manuel Akanji 22. (Ruhr Nachrichten - in German)
Meneja wa Leicester Claude Puel anasema hana hofu kwa kundoka mwezi huu kwa mAlgeria Riyad Mahrez, 26, (Leicester Mercury)
AC Milan wanasema kuwa kuwa hawawezi kumuuza kiungo wa kati mHispania Suso 24, hata kwa pauni milioni 71. (AC Milan website - in Italian)
Mesut OzilHaki miliki ya picha
Image captionMesut Ozil
Liverpool wapo tayari kupambana na Manchester City na Manchester United katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 29. (Sunday Mirror)
Pamoja na kutaka kumsajili Sanchez, Manchester United pia wanataka kumsajili Mesut Ozil, 29. (Sunday Mirror)

Manchester United wamempa Alexis Sanchez hadi siku ya Ijumaa kuamua kama anataka kwenda Old Trafford au la, vinginevyo wataachana naye. (Sunday Express)

No comments:

Post a Comment