Tuesday, 9 January 2018

Tetesi zote za Soka kutoka barani Ulaya hii leo.

Image result for Alexis Sanchez
Manchester City wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 29, na wanaamini kuwa Arsenal watamruhusu raia huyo wa Chile kuondoka mwezi huu.

Sanchez yuko tayari kurejesha kima cha pauni milioni 25 kuhakikisha kuwa amejiunga na Manchester City mwezi huu. (Sun)
Arsenal watamruhusu Sanchez kuondoka ikiwa watapokea hadi paui milioni 30 na wanataka shughuli hiyo kukamilika mapema ili kuwawezesha kumtafuta mchezaji ambaye atachukua mahala pake. (Mirror)
Taarifa zinasema kuwa Sanchez huenda akajiunga na Manchester City kwa muda wa wiki moja inayokuja. (Independent)
Arsenal wamemuorodhesha mshambuajia wa Monaco Thomas Lemar, 22, kuwa nambari moja katika kuchukua mahala pake Sanchez, baada ya kushindwa kumsaini mfaransa huyo msimu uliopita. (Mirror)
Thomas LemarHaki miliki ya picha
Image captionThomas Lemar
Meneja wa Monaco Leonardo Jardim hajakana kuwa kuuzwa kwa Lemar mwezi huu. (L'Equipe - in French)
Arsenal na Liverpool wana nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 29, ambaye anataka kuondoka kufuatia kuwasili kwa Philippe Coutinho. (Diariogol - in Spanish)
Liverpool wametupilia mbalia madai kutoka Barcelona kuwa kuuzwa kwa Coutinho kwa pauni milioni 142 kulifanyika baada ya Liverpool kupunguza fedha hizo. (Times)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Francis Coquelin, 26, ataondoka Arsenal mwezi huu, huku nao West Ham wakiwa na hamu ya kumsaini (Mirror)
Francis CoquelinHaki miliki ya picha
Image captionFrancis Coquelin
Valencia nao wako kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu Coquelin. (Cadena Ser - in Spanish)
Chelsea wamesitisha mikakati kwa kumwinda beki wa Juventus Mbrazil Alex Sandro, 26, kwa sababu klabu hiyo ya Italia inataka paunia milioni 60 kwa beki huyo. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 24, anasema yuko sawa katika klabu hiyo lakini ni lazima waanze kushinda vikombe kumwezesha kubaki. (Star)
Leicester wana nia ya kumuchia mshambuliaji Kelechi Iheanacho, 21, kuondoka mwezi huu licha ya kumsani mnigeria huyo tu hivi karibu kwa pauni milioni 25. (Sun)
Harry KaneHaki miliki ya picha
Image captionHarry Kane
West Ham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa England na Newcastle Jonjo Shelvey, 25, kwa pauni milioni 12. (Express)
Juventus hawatamsaini kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 22, kwa sababu Paris St-Germain wanataka kutoa pauni milioni 150 kwa raia huyo wa Serbia ambaye pia amewavutia Manchester United. (Il BiancoNero - in Italian)
Newcastle watamruhusu mshambuliaji raia wa Serbia Aleksandar Mitrovic, 23, kuondoka Januari lakini wanataka kurejesha pauni milioni 18 walizotumia kumnunua miezi 18 iliyopita

No comments:

Post a Comment