Mbowe amesema kuwa kauli mbalimbali alizotoa Lowassa jana si msimamo wa chama chake na kudai kuwa amesikitishwa na kauli za kiongozi huyo kuisifia Serikali ambayo wao wanaona hajatenda hata hayo ambayo amejaribu kuyasifia.
"Siyasemi haya kubishana na kauli alizozitoa Mhe. Lowassa, pengine yeye anazo takwimu zake tofauti ambazo tunazijua kwa sababu amezungumzia kuhusu ajira lakini hakusema kutolewa kwa ajira ngapi? Japo imelinganishwa na ujenzi wa reli ya kati unaweza ukaongeza ajira, Naona kuna tatizo kubwa la ajira katika nchi, na kuna ongezeko kubwa la vijana wengi ambao hawana ajira, tunatambua wanamaliza Shule hawapati ajira, lakini vile vile kuna makampuni yanafungwa, biashara zinafungwa, benki zinaelekea kufungwa nafasi nyingi za ajira zinapotea" alisema Mbowe
Aidha Mbowe aliendelea kusisitiza na kuonesha masikitiko yake kwa kauli ya Lowassa jana "Nisikitike tu kwamba sisi tuna kilio kikubwa, utakumbuka kwamba tunaendelea kumtibu Mhe. Tundu Lissu ambae alishambuliwa kwa risasi, unashindwa kupata ujasiri wowote, kiongozi wa CHADEMA kweli unamsifia Magufuli, wakati tunauguza watu, msaidizi wangu Ben Sanane amepotea, viongozi wetu wameuawa, wengine wamefungwa, Wabunge wanafukuzwa Bungeni, wakina Ester Bulaya, Halima Mdee kwa mashtaka ambayo ni ya kubambikiza ambayo hayafuati kanuni za Bunge" alisisitiza Mbowe
Mbali na hilo Freeman Mbowe ametoa kauli ambayo huenda ina ashiria kiongozi huyo kutaka kurudi kwenye chama chake cha awali CCM na kuachana na CHADEMA
"Kuhama watu kutoka chama kimoja kwenda chama kingine, haijawa jambo geni kwenye siasa za Tanzania, kazi ya kujenga Upinzani katika Taifa letu sio tukio la siku moja ni mchakato wa muda mrefu, lazima ipitie vipindi mbalimbali ambapo linafanya mchujo wa asili na kubakiza watu wachache ambao watasonga mbele wataleta uhuru wa kweli Maendeleo ya kweli na haki zote za kidemokrasia katika Taifa" alisema Mbowe
No comments:
Post a Comment