Wednesday 10 January 2018

Tetesi zote za soka kutoka barani Ulaya leo Jumatano

Related image
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hataki kuwasajili wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho licha ya kuwa nyuma ya viongozi wa ligi ya La Liga Barcelona.. (Reuters)

Manchester City wameipatia Arsenal dau la £20m ili kumsajili Alexis Sanchez, 29, huku mshambuliaji huyo wa Chile akidaiwa kukubali malipo ya £250,00 kwa wiki..(Guardian)
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anatarajiwa kuilipa Boca Juniors kitita cha pauni milioni 27 kumsajili Cristian Pavon katika ligi ya premia. (TyC Sports - in Spanish)
Cristian PavonHaki miliki ya picha
Image captionCristian Pavon
Wakati huohuo, Wenger anatarajiwa kukaa katika viti vya mashabiki katika uwanja wa Stamford Bridge kwa mechi ya Jumatano ya nusu fainali ya kombe la Carabao baada ya kupigwa marufuku ya kukaa katika eneo la wakufunzi (Express)

Zlatan Ibrahimovic
Image captionZlatan Ibrahimovic
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic huenda akaondoka Old Trafford kabla ya kukamilika kwa msimu huu.
Raia huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 36 hana kandarasi na klabu hiyo. (Yahoo Sport)
Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot
Image captionMshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot
Everton imetoa chanagamoto kwa Southampton katika ushindani wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 28, kwa dau la £20m. (Mail)
Liverpool na Arsenal watalazimika kulipa takriban £90m kumsajili mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar, 22. (Mirror)
Lakini kulingana na mwandishi wa Ufaransa Julien Laurens, huenda akachelewesha uhamisho wake Liverpool kutokana na michuano ya kombe la dunia (5 live's Euro Leagues podcast)
Thomas Lemar wa Monaco anasakwa na klabu za Liverpool na Arsenal
Image captionThomas Lemar wa Monaco anasakwa na klabu za Liverpool na Arsenal
Winga wa Brazil Lucas Moura, 25, amekubali kujiunga na Manchester United kutoka Paris St-Germain, ijapakuwa kitita cha uhamisho huo hakijakubalika kati ya vilabu hivyo viwili. (Gazetta dello Sport - in Italian)
Arsenal itawasilisha rasmi ombi jipya la kandarasi mpya ya kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuanza mazungumzo na Arsenal katika kipindi cha wiki moja ijayo na atalazimika kupunguza mshahara wake ili kusalia klabu hiyo. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere
Image captionKiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere
Borussia Monchengladbach bado imejiandaa kumsajili beki wa West Ham Reece Oxford.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 aliichezea mara nne klabu hiyo wakati alipokuwa katika mkopo lakini alirudi katika klabu yake mwezi Disemba. (Borussia Monchengladbach)
Na West Ham huenda ikamuuza beki wa Uingereza iwapo ligi ya Bundesliga imejiandaa kuongeza ombi lake la £15m. (Telegraph)
Michy Batshuayi
Image captionMichy Batshuayi
Klabu ya Uhispania ya Sevilla ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, 24, kwa mkopo. (ESPN)
Lakini mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amesema anafuraha anampenda mchezaji huyo wa Ubelgiji ambaye ameichezea Chelsea mara mbili pekee. (Sky Sports)

No comments:

Post a Comment