Chelsea imemsajili mshambuliji wa Arsenal Olivier Giroud kwa mkataba wa miezi 18 utakaogharimu £18m.
Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31, anaondoka arsenal baada ya kufunga mabao 105 katika mechi 253 tangu asajiliwe kutoka klabu ya Ufaransa ya Montpellier kwa kitita cha £12m mnamo mwezi Juni 2012.
Borussia Dortmund pia wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi hadi mwisho wa msimu huu.
Awali Dortmund ilimuuza Pierre-Emerick Aubameyang kwa Arsenal.
Wakati huohuo Manchester City wamejiondoa katika makubaliano ya kumsajili winga wa Leicester Riyad Mahrez wakidai kwamba uhamisho wake ungeigharimu klabu hiyo dau kubwa la £95m.
Siku ya Jumanne mchezaji huyo alikuwa amewasilisha ombi la kuondoka katika klabu yake ya Leicester
Borussia Dortmund imekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi kwa mkopo kwa kipindi cha msimu uliosalia, akisubiri kufanyiwa matibabu.
Wakati huohuo kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil ametia saini kandarasi ya miaka mitatu na nusu ili kusalia katika klabu hiyo hadi 2021.
Ozil mwenye umri wa miaka 29 sasa ndio mchezaji anayepokea mshahara mkubwa katika klabu hiyo akijapatia kitita cha £350,000 kwa wiki kabla ya kulipa kodi.
Mkataba huo uliotiwa saini siku ya Jumatano, unajiri baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatma ya raia huyo wa Ujerumani ambaye kandarasi yake ya awali ilikuwa inakaribia kuisha mwishoni mwa msimu huu.
Alijiunga na Gunners kutoka Real Madrid 2013 kwa rekodi ya uhamisho wa dau la £42.4m.
No comments:
Post a Comment