Wednesday 7 February 2018

Alichokisema Kipa wa Azam FC Razack kuhusu Okwi na John Bocco.


Related image
Kipa wa Azam FC, Razack Abarola raia wa Ghana ameweka wazi kuwa amejipanga kikamilifu kuisaidia timu yake kuibuka na matokeo mazuri mbele ya wapinzani wao Simba kwa kuzuia mabao ya washambuliaji wa Simba wakiongozwa na John Bocco na Emmanuel Okwi.

Leo Jumatano Azam FC ambao walishinda kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Ndanda FC watakuwa na jukumu zito la kuwakabili Simba ambao ndiyo vinara wa ligi hadi sasa kwenye pambano litakalokuwa na ushindani lililopangwa kupigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mghana huyo ambaye anashika nafasi ya pili katika orodha ya makipa waliocheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao mechi 10, amesema kwamba lengo lake ni kuona analinda ngome yake vizuri na kutofungwa bao lolote katika mchezo huo dhidi ya Simba.
Related image
Kipa wa Azam FC, Razack Abarola
“Tunatambua wao ni wazuri lakini sisi ni wazuri na tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata pointi tatu na kuwasogelea katika mbio za ubingwa kwani kama unavyojua wao ndiyo wapo juu yetu lakini sisi tutapambana kupata matokeo na pointi tatu.

No comments:

Post a Comment