Wednesday 7 February 2018

Kocha wa Singida United Hans Pluijm aweka wazi lengo lake msimu huu.

Image result for Pluijm singida united
Bosi mkuu wa benchi la ufundi la Singida United, Hans van Der Pluijm raia wa Uholanzi, amefunguka kuwa azma yake ni kukiona kikosi hicho kinapanda ndege kwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho (FA).

Mholanzi huyo amesema hayo wakati wiki iliyopita alikiongoza kikosi chake kutinga hatua ya 16 Bora ya Kombe hilo baada ya kuifunga Green Warriors kwa penalti 4-3, kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Kocha huyo ambaye kikosi chake kinashika nafasi ya nne kwenye ligi kuu kikiwa na pointi 30 amesema mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha anaipatia timu hiyo nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa ambapo lengo lao ni kutwaa ubingwa wa FA ambao unaonekana kuwa rahisi kuliko kwenye ligi.

“Tunashukuru hadi hapa tulipofika kwenye michuano hii ya FA, ambapo lengo letu kama litakamilika ni kuchukua ubingwa wa kombe hili ili tujikatie nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, ambapo hilo ndilo lengo kwa msimu huu.

“Ujue njia ya kutinga michuano ya kimataifa ni rahisi sana kwa kupitia huku kwenye Kombe la Shrikisho (FA) kuliko ligi ambapo kwa sasa kumekuwa na ugumu sana japo tunaendelea kupambana, tutaendelea kufanya vizuri katika kila mchezo wetu wa kombe hili ili mwisho tukamilishe malengo yetu,” alisema Pluijm.

No comments:

Post a Comment