Kikosi cha Yanga, kimeeleza kipo tayari kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Njombe Mji jijini Dar es Salaam, leo.
Mechi hiyo itakuwa ni ya pili ya Yanga katika mzunguko wa pili baada ya kuuanza vizuri kwa ushindi katika mechi ya kwanza dhidi ya Lipuli FC.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema kikosi chake kimeendelea na maandalizi mara tu baada ya mechi dhidi ya Lipuli.
“Pamoja na kushinda, mechi inapoisha lazima kunakuwa na makosa ambayo tunayafanyia kazi na kuanza kazi nyingine upya.
“Hivyo tumeangalia tulipokosea na kufanya marekebisho na sasa tuko tayari kuendelea kupambana,” alisema.
Yanga imekuwa ikiandamwa na majeruha mfululizo katika kikosi chake ingawa imeendelea kupambana ikichuana na Azam FC na vinara Simba wanaoonekana kuwa na kasi kubwa.
No comments:
Post a Comment