Tuesday, 6 February 2018

Mwamuzi Jonesia Lukyaa aondolewa kuchezesha mechi ya Simba VS Azam FC

Image result for simba vs azam fc mapinduzi cup
Mwamuzi Jonesia Lukyaa aliyekuwa achezeshe mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Azam FC, amebadilishwa.

Simba na Azam FC ambazo zinachuana kileleni mwa Ligi Kuu Bara, zinavaana kesho katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.

Taarifa zinaeleza mwamuzi huyo mwanamama mwenye beji ya Fifa amebadilishwa na nafasi yake amepewa mwamuzi mwingine.

“Nafasi yake amepewa Emmanuel Mwandengwa, hivyo hatachezesha,” kilieleza chanzo.

Hata hivyo, hakukuwa na ufafanuzi kuhusiana na suala hilo la uamuzi wa kumbadili siku chache kabla ya mechi.

No comments:

Post a Comment