Simba ambayo imevuna mabao 15 katika mechi tano zilizopita huku ikiwa haijaruhusu bao kwenye michezo hiyo ya hivi karibu na kuifanya hadi sasa kucheka na nyavu mara 38 kufuatia kushuka dimbani mara 16 tangu kuanza kwa Ligi msimu huu imeeleza siri ya mafanikio hayo.
Kocha msaidizi wa timu hiyo Mrundi masoud Djuma amedokeza siri ya mafanikio hayo wanayoendelea kuyapata kuwa yanatokana na mbinu zao za uchezaji zinazowafanya wapinzani wao kushindwa kuendana na kasi yao.
"kucheza mbali na lango letu kwa maana ya kucheza na eneo la adui linatupa nafasi kubwa yakujilinda na kupata mabao na kucheza zaidi kwenye lango la adui kuna muongezea presha mpinzani wetu na ikitokea akafanya makosa kidogo tunamuadhibu ,lakini pia tumekuwa tukibadilika badilika katika kila mchezo" aliongeza Djuma
No comments:
Post a Comment