Mshambuliaji wa Lipuli FC ya Iringa, Malimi Busungu, amemtaja Obrey Chirwa kuwa ndiye aliyewavuruga zaidi kwenye mchezo wao wa juzi Jumamosi na kujikuta wakipoteza kwa mabao 2-0.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Pius Buswita na Papy Tshishimbi.
Busungu amesema pamoja na kwamba Chirwa hakufunga, lakini ndiye aliyekuwa mwiba kwao muda wote wa dakika tisini za mchezo huo.
“Mchezo ulikuwa mgumu ingawa tulijipanga vizuri kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye uwanja wetu wa nyumbani, lakini haikuwa hivyo, tumekubali matokeo.
“Kiukweli mchezaji wa Yanga ambaye alichangia kuvuruga mipango yetu ni Chirwa kutokana na kwamba ile mipira aliyokuwa akiipata alikuwa akiisumbua sana ngome yetu ya ulinzi na ingawa hakufunga lakini alikuwa hatari,” alisema Busungu.
No comments:
Post a Comment