Monday, 5 February 2018

Tetesi zote za soka kwa siku ya Leo Jumatatu Februari 5.

Related image
Klabu ya Liverpool itaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, kama mchezaji huyo atagoma kusaini mkataba mpya na klabu yake.

Manchester United wanamfutilia kwa karibu kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic ili kuweza kumsajili kiungo huyo katika dirisha kubwa la usajili.
Mshambuliji wa Man United Marcus Rashford anaweza kuondoka klabuni hapo ikiwa United wa tamsajili Justin Kluiverts kutoka Ajax.
EPLHaki miliki ya picha
Image captionWinga wa Bordeaux Malcom Oliveira
Mshambuliaji wa Kibrazil Malcom Oliveira, anataka kuondoka katika klabu yake ya Bordeaux, na Mchezaji huyo anawinda na Tottenham na Arsenal
Mshambuliji wa West Ham Javier Hernandez, 29, amesema atajitoa kwa asilimia mia moja katika klabu yake licha ya kutaka kuondoka klabuni hapo katika dirisha la mwezi januari
Mfaransa Olivier Giroud mwenye miaka 31 ambae anaweza anza katika mchezo wa timu yake mpya ya Chelsea itapocheza na Watford amesema alipewa motisha ya kuhama na kocha wa timu ya taifa ya ufaransa Didier Deschamps.
eplHaki miliki ya picha
Image captionMshambuliaji mpya wa Chelsea Olivier Giroud
Winga wa Leicester Marc Albrighton amekanusha taarifa zinazozagaa mitandaoni kuwa wachezaji wa Foxes wanahasira na mchezaji mwenzao Riyad Mahrez aliyetaka kuhama na kujiunga na Man City.

No comments:

Post a Comment