Saturday 17 February 2018

Emmanuel Okwi atoa ahadi ya kwa mashabiki wa Simba.

Image result for Emmanuel Okwi
Baada ya kufunga bao la kwanza nje ya Dar es Salaam, straika wa Simba, Emmanuel Okwi amesema kuanzia sasa ataendelea kufunga katika kiwanja chochote kile atakachocheza akipata nafasi.

Juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Okwi aliifungia Simba bao la pili kwa penalti dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.

Hilo lilikuwa bao la kwanza kwa Okwi kufunga nje ya Dar es Salaam kwani katika mabao 13 aliyofunga awali, yote aliyafunga katika viwanja vya Taifa na Uhuru jijini Dar es Salaam.

“Nitaendelea kufunga mabao kwani mchezo wa Mwadui umenifungulia njia, namshukuru Mungu kuona nimefunga bao mkoani.

“Niwaahidi mashabiki wa Simba kuwa nitaendelea kupambana ili niweze kupata mabao mengi zaidi kabla ya ligi kuisha, kufunga bao mkoani si kitu kidogo kwani huwa tunakamiwa kupita kiasi.

“Naamini mimi kuanza kufunga tena kwa penalti, ni hatua nzuri ambayo naamini itanisaidia kufanya vizuri ili niweze kuibuka na ufungaji bora wa ligi kuu.”

Okwi sasa amefikisha mabao 14 katika orodha ya wafungaji bora na ndiye anaongoza kwa ufungaji akifuatiwa na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa mwenye mabao 11 halafu nafasi ya tatu yupo John Bocco wa Simba mwenye mabao 10.

No comments:

Post a Comment