Saturday 10 February 2018

Jonas Mkude afunguka dawa ya kumaliza matumaini ya Yanga kuchukua Ubingwa.

Related image
Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude, amesema wanashukuru kwa sasa wana kikosi bora chenye mafanikio wanayoendelea kuyapata na kudai kuwa wanahitaji kushinda kila mechi hivyo wapinzani wao Yanga wakae pembeni.


Simba inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 41 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 34. Yanga ndiyo bingwa mtetezi wa ligi hiyo.

Mkude alisema wamejipanga kufanya vizuri katika kila mechi ili wapinzani wao Yanga wasiwafikie kutokana na upinzani uliopo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.

“Tunashukuru tumefanikiwa kushinda mchezo wetu na Azam hivyo kwa sasa mtazamo wetu ni kuona tunafanikiwa kushinda katika michezo iliyobakia ili kujiweka katika nafasi nzuri na kukaa mbali na wapinzani wetu Yanga.

“Moja ya malengo yetu ni kuona tunafanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu kwa kufanya vizuri katika kila mechi,” alisema Mkude.


Alisema wamejiandaa vizuri kushinda mechi ya kesho ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Djibouti ili waweze kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment