Saturday 10 February 2018

Walichokisema Mabingwa wa Shelisheli kuhusu kumuofia Obrey Chirwa wa Yanga

Image result for obrey chirwa yanga
Mabingwa wa Shelisheli, St Louis kuna namna fulani hivi, pamoja na kujitapa wanaonekana wameingia hofu fulani hivi.

Timu hiyo leo inashuka dimbani katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwavaa mabingwa wa Tanzania, Yanga.

Hofu ya St Louis inaonekana iko kwa safu ya ushambulizi ya Yanga hasa Mzambia, Obrey Chirwa.

Mkurugenzi wa Ufundi wa St Louis, Ulrie Mathiot, amesema wamemuona Chirwa kupitia video za mechi za Yanga za nyuma ikiwemo ile ya hivi karibuni dhidi ya Azam FC.

Mathiot alisema wamebaini Chirwa ndiye mchezaji atakayewasumbua katika mchezo huo utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Mchezaji huyo tumemuona ana nguvu, kasi, pia anajua kufunga, kwa hiyo nahisi huyo ndiye atakayetusumbua.
“Lakini wachezaji wengine tumewaona kuwa ni wa kawaida, hawatishi kama alivyo mshambuliaji huyo ambaye tumeambiwa kuwa ni raia wa Zambia,” alisema Mathiot.


Kwa upande wake, Chirwa akizungumzia mchezo wa leo, alisema atahakikisha anapambana vilivyo ili aweze kuisaidia Yanga kupata ushindi kwa sababu kufunga ndiyo kazi anayotakiwa kuifanya.


“Sikuja Yanga kufanya kazi nyingine tofauti na soka, kwa hiyo nitapambana kuhakikisha naipatia ushindi timu yangu katika mechi hiyo na nyingine,” alisema Chirwa mwenye mabao kumi kwenye Ligi Kuu Bara.


No comments:

Post a Comment