Thursday 22 February 2018

Kocha wa Simba Pierre Lechantre awambia ukweli wachezaji wake kuhusu Al Masry asisitiza kazi ipo.

Related image
Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amesema anakijua kikosi cha Al Masry cha Misri, lakini akaonya.


Simba itakutana na Al Masry mwanzoni mwa mwezi Machi katika mechi ya Kombe la Shirikisho, timu zikianzia Dar es Salaam.

Lechantre raia wa Ufaransa amesema timu hiyo si ya kubeza, ngumu na inahitajika maandalizi ya kutosha.

Kocha kuyo amesema: “Hakuna kisichowezekana, tuna kikosi kizuri na tuna uwezo wa kuwatoa. Lakini haiwezi kuwa rahisi.

“Lazima tujiandae vizuri, tufanye kazi kwa uhakika na ninaamini tutafanya vizuri.”


Kocha huyo amewahi kufanya kazi nchini Tunisia na nchi nyingine mbalimbali za Ukanda wa Afrika Kaskazini na barani Asia.


No comments:

Post a Comment