Thursday 22 February 2018

Yaliojitokeza katika Hospitali ya Muhimbili wakati wa kuchukua Mwili wa Akwelina.


VILIO na simanzi vimetawala wakati wa kuchukua mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini aliyeuawa kwa kupigwa risasi Feb 16, 2018.

Mwili wa Akwilina umechukuliwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupelekwa NIT k wa ajili ya kuagwa kabla ya kupelekwa nyumbani kwao Rombo kwa mazishi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa anaongoza msafara wa magari, likiwemo lililobeba mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuelekea katika viwanja vya chuo hicho kwa ajili ya kuagwa.

Jeneza lenye mwili wa mwanafunzi huo liko katika gari maalumu la kubebea maiti.

No comments:

Post a Comment