Thursday 8 February 2018

Sallam SK afichua mazito kuhusu Ugomvi baina ya WCB na Ruge Mutahaba.



Meneja wa label ya WCB, Sallam SK amefunguka kwa kuendelea kudai kwamba kampuni yao haina tatizo na chombo chochote cha habari isipokuwa Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds FM na Clouds TV ndio mwenye tatizo na label hiyo.


Mapema wiki hii meneja huyo alianza kwa kuandika ujumbe mtandaoni unaodai kuna mtu anataka kumshusha Diamond huku akidai hakuna mtu wa kumshusha katika utawala huu wa Rais John Pombe Magufuli.
Image result for Sallam SK
Sallam SK
Sallam ameendeleza mashambulizi hayo ambapo jana amemtaja mtu aliyedai kwamba ana njama za kumshusha Diamond.
Baadhi ya Wasanii wa kundi la WCB
“Kwa heshima ya Joe Kusaga kukuombea msamaha kwa leo Bw Ruge Mutahaba naamua kukusitiri, ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi nitayaanika maovu yako yote unayoyafanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds Media Group ila huyu Ruge Mutahaba ndio mwenye tatizo #TumekataaKuwaKaa,” aliandika Sallam kupitia Instagram.
Image result for RUGE MUTAHABA
Ruge Mutahaba Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds FM na Clouds TV
Meneja huyo anaonekana kutaka kuendeleza harakati hizo kwani toka aanze kutoa waraka huo amekuwa akiweka hushtag ambayo imekuwa ikitumika na Clouds Media, #TumekataaKuwaKaa.

No comments:

Post a Comment