Thursday 8 February 2018

Vanessa Mdee ataja mtonyo alioingiza mpaka sasa mauzo ya Albam yake.



Vanessa Mdee amesema mpaka sasa ameuza nakala zaidi ya elfu 4 na kila nakala moja anaiuza kwa shilingi elfu 10 ambapo kwa mahesabu ya haraka haraka ameingiza zaidi ya shilingi milioni 40 ndani ya mwezi mmoja.


Namshukuru Mungu tumeshauza nakala zaidi ya elfu nne za CD ya #MoneyMondaysTheAlbum kwa sasa tupo Zanzibar kuendelea na mauzo. Asanteni Sana kwa support yenu. Let’s get to 10,000 copies in less than a month. Usinunue CD ya #moneymondays isiyokuwa na sticker ya TRA.“ameandika Vanessa Mdee kwenye ukurasa wake wa Instagram.

No comments:

Post a Comment