Friday 9 February 2018

Watu wasiojulikana wamvamia Wema Sepetu wachukua mamilioni.

Wiki moja baada ya akaunti ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu kudukuliwa na watu wasiojulikana , mrembo huyo anadaiwa kupigwa mamilioni.


Habari zilizolifikia  zilieleza kuwa, tangu mrembo huyo adukuliwe akaunti yake  yenye wafuasi zaidi ya milioni tatu, na watu wasiojulikana  wamekuwa wakiitumia ndivyo sivyo kwa kuposti matangazo mbalimbali ya kibiashara ambapo wanachukua pesa bila ya Wema kujua.

Account ya Wema Sepetu ya Instagram

Inaelezwa kuwa, Wema alikuwa akitumia akaunti hiyo kupitia namba ya simu ya mtandao maarufu wa mawasiliano nchini ambapo wadukuzi walifanikiwa kumiliki namba hiyo ambayo hutumia moja kwa moja kuwasiliana na wafanyabiashara mbalimbali wa mtandao kwa mgongo wa Wema na kuvuna pesa.

Meneja wa Wema, Neema Ndepanya  baada ya kuelezwa taarifa hizo alifafanua kuwa, jambo hilo lipo mikononi mwao na kwamba kuna vijana wawili wanaofanya kazi kwa ukaribu na Wema, Bestizo na mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda ambao wanafuatilia kwa ukaribu.

“Ni kweli kabisa mpaka sasa Bestizo na Kadinda wanafuatilia kwenye mtandao wa simu (anautaja) kujua kwa nini wameshindwa kuthibiti suala hilo hadi sasa ambapo matapeli wanatumia njia kuwaibia watu kupitia akaunti hiyo,” alisema Neema.

No comments:

Post a Comment