Mkufunzi wa Brazil Tite amesema timu yake bado inatatizwa na "mizimu" ya kipigo cha 7-1 ambacho walipokezwa na Ujerumani katika nusu fainali ya Kombe la Dunia miaka minne iliyopita.
Mataifa hayo mawili yatakutana tena wka mara ya kwanza Jumanne mjini Berlin tangu Brazil walipoaibishwa kwao nyumbani wakati wa michuano hiyo ya Kombe la Dunia.
"Hii ina maana kubwa sana kisaikolojia - hakuna anayehitaji kujidanganya kuhusu hilo," Titea aliambia jarida la Kicker.
"Matokeo hayo ya 7-1 ni kama mizimu, watu bado huyazungumzia. Kadiri unavyoyazungumzia zaidi, ndivyo mizimu hii inavyochukua muda mrefu kutoweka."
Toni Kroos alifunga mabao mawili wakati huo naye Miroslav Klose akavunja rekodi ya ufungaji mabao Kombe la Dunia mwaka 2014 Ujerumani walipoafanikiwa kujiweka mbele 5-0 dakika 29 za kwanza kwenye nusu fainali hiyo.
Katika mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki itakayochezewa Berlin, kiungo wa kati wa Manchester City Fernandinho anatarajiwa kuingia uwanjani nafasi ya Douglas Costa.
Hilo litakuwa ndilo badiliko pekee kwenye timu ambayo ililaza Urusi 3-0 mjini Moscow mnamo Ijumaa bila nyota wao Neymar ambaye anauguza jeraha.
"Nilikuwa ninatazama mechi hiyo (ya mwaka 2014) niliwa nyumbani Sao Paulo na mke wangu na baada ya bao la tatu kufungwa, alianza kulia," amesema Tite.
"Hili lilinigusa sana, nami nikaanza. Ulikuwa wakati mzuri sana kwa Ujerumani, kila kombora lililolenga goli lilikuwa bao - mambo kama hayo huwa hayatokei hata kwenye michezo ya video ya kompyuta.
"Kidonga hicho bado hakijapona na Berlin ni sehemu ya mchakato wa kukiponya kabisa."
Meneja wa Ujerumani Joachim Low alimpumzisha nyota wa Arsenal Mesut Ozil na mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller for kwa ajili ya mechi hii.
Kevin Trapp na Bernd Leno walichezeshwa dakika 45 kila mmoja langoni.
Low - ambaye timu yake ni moja ya zinazopigiwa upatu kufana katika Kombe la Dunia Urusi baadaye mwaka huu - amesema: "Huenda kukawa na wachezaji watatu au wanne waliokuwa kwenye kikosi cha 2014 watakaoanza mechi leo.
"Bila shaka, Wabrazil wanataka sana kulipiza kisasi, lakini hauwezi kurudisha saa nyuma na kufuta yaliyotokea."
"7-1 ni yaliyopita."
No comments:
Post a Comment