Kutokana na kauli zilizohusisha kabila la Wachaga (kwamba ni ajabu Mchaga kutoa fedha kusaidia walemavu) zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa kumuaga Reginald Mengi katka Ukumbi wa Karimjee, Katibu Mku wa CCM Dkt Bashiru alisema anaomba msamaha kwa niaba ya RC Paul Makonda.
“Baba Askofu hatujafanya kazi ya kuwaandaa vijana wetu kuwa Viongozi bora, sasa tunavuna matunda yake, naomba nimuombe msamaha kijana wangu Makonda, nilimsema Simiyu mara ya kwanza, akaja ofisini analia, ameanza kujirekebisha.
“Naomba nimuombee msamaha kijana wangu Makonda, hii ni mara yangu ya pili nimemsema hadharani”. Bashiru Ally Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi,” amesema Dkt. Bashiru.
Baada ya hapo, Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliwaita RC Makonda na Freeman Mbowe akisema hiyo ni ishara ya kusameheana na mariadhiano na kuwataka wapeane mikono. Baada ya kupeana mikono RC Makonda alizungumza na kusema hakuwa na nia mbaya ila tafsiri imeleta shida hivyo anaomb radhi ‘kutokana na tafsiri’.
“Namshukuru Katibu Mkuu kwa kuomba radhi kwa niaba yangu, hakika ni upendo wa hali ya juu. Ninahisi tafasiri inaweza kuwa ni tatizo na mimi niombe radhi kwa tafsiri hiyo kwa sababu nimemsifia mchaga katikati ya wachaga sio mchaga tofauti na kabila jingine. Napokea na nitaendelea kumuenzi Mzee Mengi kwa mema yote aliyoyafanya hasa kwa mkoa wetu kuwahudumia walemavu sababu amekuwa alama ambayo daima haitafutika,” amesema Makonda.
Awali Mbowe aliwataka Watanzania kutogombanishwa na kauli za viongozi hasa za kikabila na kidini huku akiwataka viongozi kutafakari maneno kabla ya kuyaongea kwani yanaweza kugawa watu na
“”Kipekee kabisa na mnisamehe jambo moja ambalo limetukwaza wengi, akitokea Kiongozi akitoa akatoa kauli ya kubeza kabila fulani, tukaanza kubaguana kwa Makabila au Dini sio mambo mema, tuungane kukemea. Kuna kauli zinasemwa sana watu na kwa ukweli zinakera kwa vile mimi si mnafiki lazima niseme na nitasema hapahapa mbele za watu.
“Tuna nchi moja ambayo tunastahili kupendana na kusaidiana, na kila mtu ana haki ya kumsaidia mwenzie, tusikubali kauli za viongozi zitugawe na hasa za kidini na kikabila, kauli ya kusema kuna makabila hayawezi kuwasaidia walemavu si nzuri na haikutupendeza kwa kweli, tujitafakari tunapotaka kuongea maneno,” amesema Mbowe.
No comments:
Post a Comment