Wednesday 8 May 2019

SIMBA YAWAPA COASTAL KIPIGO CHA MBWA KOKO BAO 8-1 NA KUPANDA KILELENI


KLABU ya Simba imetinga kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuipiga kipigo hevi cha bao 8-1, timu ya Coastal Union ya Tanga leo Jumatano, Mei 8, 2019.

Mabao ya Simba Sc

Emmanuel Okwi (dakika ya 11′, 20′ na 47′)
Meddie Kagere  (dakika ya 69′, 75′ na 83′)
Hassan Dilunga (dakika ya 81′)
Clatous Chama (90+2)

Bao pekee la Coastal Union limefungwa na ⚽Raizan Hafidh (dakika ya 35). Raizin Hafidh ndio alifunga bao pekee wakati Simba ikishinda 2-1 dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani. Leo amefunga tena dhidi ya Simba.

Okwi amefikisha magoli 13 kwenye ligi msimu huu, anawakimbiza Heritier Makambo (16), Salim Aiyee (16) na Meddie Kagere (17)

Rekodi ya Simba msimu huu.

🏟Mechi 31
🧾Pointi 81
✔Ushindi 26
🤝🏼Sare 3
❌Vipigo 2
⚽Magoli ya kufunga 69
🥅Magoli ya kufungwa 13.

No comments:

Post a Comment