Wednesday 7 August 2019

MASTAA 9 WANAOMILIKI VISIWA DUNIANI.


KUMILIKI eneo ambalo unaweza kupata burudani, ukalima chochote unachokitaka na kufurahia maisha na familia yako ni moja ya ndoto zilizotimia za mastaa maarufu duniani ambao wanamiliki visiwa kwa ajili ya kukonga nyoyo zao.  Mastaa hao ni wafuatao:


1. Mel Gibson
Staa huyo mkongwe wa  Australian,  Mel Gibson, anamiliki kisiwa cha Mago chenye hekta elfu tano alichokinunua kwa Dola milioni 15 miaka 15 iliyopita. 

2. Ricky Martin
Miaka 11 iliyopita, Ricky Martin, alinunua kisiwa cha Angra dos Reis nchini Brazil kwa dola milioni nane kwa ajili ya kujinafsi. 

3. Shakira
Mwanamama Shakira anamiliki hekta 700  za kisiwa cha Bonds Cay  nchini Bahamas,  kilichomgharimu Dola milioni 16.

4. Nicholas Cage
Staa huyo, Nicolas Cage, anamiliki  hekta 40 za kisiwa cha  Leaf Cay island (Bahamas) alichokinunua kwa Dola milioni tatu tu.

5. Johnny Depp
Staa huyo anamiliki hekta 45 za kisiwa kiitwacho  Little Halls Pond Cay, kilichomgharimu Dola mil. nne.

6. Leonardo DiCaprio
Nyota huyo alinunua kisiwa cha Blackadore Cay,  nchini Belize,  miaka mitano iliyopita kwa Dola mil. 1.8.

7. Eddie Murphy
Mkongwe wa uigizaji , Eddie Murphy, alinunua kisiwa cha Rooster Cay, Bahamas, mwaka 2007, kwa Dola mil. 15.



8. David Copperfield
Nyota huyo ana visiwa vinne nchini Bahamas vilivyomgharimu Dola mil. 50 ambapo amehakikisha vimesheheni kila aina ya burudani.

9. Brooke Shields
Mwanamama huyo anamiliki kisiwa kiitwacho Emerald Island karibu na Jiji la  New York, kikiwa na aneo la hekta 8.5. 

No comments:

Post a Comment