Wednesday 7 August 2019

Tetesi zote za Soka Ulaya Jumatano 07.08.2019


Tottenham wamefikia makubaliano na Juventus kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, kwa dau la karibu £62m. (Sky Sports Italia, via Daily Mail)


Dybala anajiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba na Tottenham kabla ya Alhamisi ambao ni muda wa mwisho uliowekwa kwa uhamisho wa wachezaji kukamilika. (Goal)

Tottenham pia wanapania kumsaini mshambuliaji wa Barcelona wa miaka 27- Mbrazil Philippe Coutinho. (ESPN)

DC United wanajiandaa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 30, wanapojaribu kujaza pengo lililoachwa wazi na Wayne Rooney anayeelekea Derby. (Mirror)
Manchester United wameongeza juhudi ya kufikia mkataba na na kiungo wa kati Tottenham Christian Eriksen, 27. (Telegraph)

Eriksen hayuko katika mpango wa wa muda mrefu wa Mauricio Pochettino, Tottenham - na tayari amethibitisha kuwa anataka changamoto mpya. (Mirror)

Uamuzi wa dakika za mwisho wa United kumhusu Eriksen unakuja licha ya tetesi ikiwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, ataendelea kuwa katika klabu hiyo hadi mwisho wa dirisha la uhamisho litakapofungwa. (Standard)

Arsenal wanaweza kuelekeza nguvu zao zote katika kumsajili beki wa kati wa RB LeipzigMfaransa Dayot Upamecano, 20, kama mbadala wa beki wa Juventus Daniele Rugani - lakini Leipzig wanataka pauni milioni 50 ili kumuachia beki huyo. (Mirror)

Leicester haitamsajili Nathan Ake katika dirisha hili la usajili baada ya klabu ya Bournemouthkutaka dau la pauni milioni 75 kwa beki huyo raia wa Uholanzai. (Sky Sports)

Arsenal wamejaribu kufikia makubaliano na nahodha wao Laurent Koscielny - lakini beki huyo mwenye miaka 33, ambaye aligoma kusafiri na timu kwenda Marekani, pia amegoma kufanya mazungumzo na klabu. (Mirror)



No comments:

Post a Comment